Thursday, April 21, 2016

""Netiweki/Network."" COMPUTER GUIDE "JIFUNZE MWENYEWE" SEHEMU YA 4

Network.

Utangulizi (Introduction):


Kuingia katika Mtandao [Logging Into The Network]
Kuingia au kufungua mashine yeyote ile ina maanisha kutaka ule mfumo ukuruhusu kuingia ndani yake nakuweza kufikia mafaili yenye kazi na habari mbali mbali, au kujiunganisha na watu wengine waliopo kwenye mtandao huo unaotaka kuingia, au kutaka kushirikiana mafaili yenye mahusiano katika mtandao huo au kutaka kuzitumia programu mbalimbali zilizomo katika mashine hiyo/yako.
Ilikuruhusiwa kuingia katika mashine hiyo haswa ya kompyuta ni lazima uwe umethibitishwa na kuruhusiwa. Hivyo basi kila mfumo utakaotaka kuingia utakuhitaji kuingia katika mtandao huo kwa kutumia jina lako la utambulisho la kipekee pamoja na namba yako ya siri (ID and password). Kila mtumiaji wa mtandao wanalazimika kuwa na jina lake la kuingilia pamoja na namba yake ya siri (Every user of the network will have their own login ID and password) MUHIMU:Usimruhusu mtu yeyote afahamu jina na namba yako ya siti.

Namna ya Kuingia katika Mtandao
(
How to Log Into The Network)
1.  Kila mara utakapokuwa unawasha kompyuta yako katika kioo cha kompyuta hiyo kutajitokeza kiboksi cha maelekezo (a login screen) kikikutaka uandike jina lako la kufungulia na namba yako ya siri (login ID and password)
2.  Katika sehemu ya Jina la Mtumiaji (Username):
andika Jina lako la kipekee (login ID)
3.  sehemu ya Namba ya Siri (Password):
andika namba yako ya siri (password) 
4.  Bonyeza kitufe kilichoandikwa Ingia/sawa (Click ok/Signin)