Tuesday, April 12, 2016

KUA MTAALAM WA KUTENGENEZA COMPYUTA

GUNDUA NA KUTATUA TATIZO LA KOMPYUTA YAKO KWA URAHISI

Kwanza kabisa kabla hujagundua tatizo ama kuanza matengenezo ni lazima uwe unajua Kompyuta ina sehemu mbili ambazo ni Hardware (vifaa vinavyoshikika) na  Sotware(vifaa visivyoshikika).Kwa hiyo tatizo linaweza kuwa katika upande wa Software au Hardware.




HATUA ZA KUKABILIANA NA UTATUZI WA TATIZO LA KOMPYUTA YAKO.
Kuna hatua kama sita unazopaswa kuzifuata ili kujua na kutatua tatizo linaloikabili kompyuta yako:

1. Ligundue tatizo. hatua ya kwanza unayopaswa kufanya kama wewe ni IT technician ni kugundua tatizo la kompyuta yako kabla hujaanza matengenezo.Kwa mfano kompyuta yako ikiwaka haioneshi chochote kwenye kioo.Kwa hiyo hapo tatizo ni kwamba haioneshi chochote kwenye kioo.
2. Pata Maelezo kutoka kwa mtumiaji wa Mwisho. Hii inakusaidia kuweza kukufanya wewe uweze kuzalisha majibu mbalimbali yanayoweza kuwa yamesababisha hilo tatizo. Kwa mfano mtumiaji anaweza kukuambia hivi"nilikuwa natumia kompyuta mara nikasikia Paa kisha nikaona moshi unatoka kwa nyuma"
3. Zalisha Njia Mbalimbali(majibu) zitakazokusaidia kutatua tatizo. Katika uzalishaji wa majibu hayo unapaswa kutumia uzoefu, utaalamu ulionao pamoja na njia mbalimbali ambazo wewe kama expert unazijua.Kama kompyuta imegawanyika katika sehemu mbili hivyo hata tatizo linapotokea ni lazima litokane na upande mmoja wapo.Hivyo IT technician anatakiwa ajue matumizi ya kifaa kimojamoja cha kompyuta.
4.  Anza Matengenezo kutoka hatua moja hadi nyingine. Hapa ndipo unapoanza kufanya matengenezo ukiwa na kifaa husika ambacho unahisi kina tatizo na unataka kukibadilisha.

Unatakiwa uanze kutatua na tatizo ambalo unahisi ni dogo kabla ya kuelekea kwenye hatua kubwa na kama unahisi kuna matatizo kama manne yanayoweza kuwa yamesababisha hilo tatizo unashauriwa kufanya kitu kimojakimoja na usifanye vyote kwa wakati mmoja.

Unashauriwa kuhamisha data za muhimu kabla ya kufanya utatuzi wa tatizo kwa sababu zinaweza kupotea
5.  Je tatizo limetatuliwa? Kama jibu limetatuliwa unarudi katika hatua ya 3 ukianza na hatua nyingine mbadala kati ya zile ulizokuwa umependekeza. Ila kama tatizo limetatuliwa na kompyuta yako imerudi katika hatua yake ya kwaida una-andika sehemu kwa ajili ya kumbukumbu.
6.  Weka kumbukumbu. Pale Technician unapokuwa umefanikiwa kutatua tatizo unashauriwa kuchapa(kuandika) hatua ulizopitia kwa ajili ya msaada wa baadae endapo utakutana na tatizo kama hilo kwa sababu matatizo ya kompyuta mara nyingi yanafanana.

By...
♻Mtz
     ✳Admin
www.dtoxengineer.blogspot.com 
e-mail
phone