Saturday, April 16, 2016

COMPUTER GUIDE "JIFUNZE MWENYEWE" SEHEMU YA 1

Kompyuta ni nini?


Swali hili lina majibu mengi kama ifutavyo:

Kompyuta ni mashine/kifaa:-
1.  Kitumikacho katika kufanyia mahesabu, kukusanya data, vilevile hutumika kukusanya, kuweka pamoja na kuzishughulikia/kuzifanyia kazi habari hizo.

2.  Kitumikacho kuandikia kazi mbalimbali na machapisho kama vile vitabu, magazeti n.k.

3.  Itumikayo kuhifadhia kazi na habari .
4.  Itumikayo kuwasiliana na kupeleka taarifa
5.  Itumikayo kutafutia habari toka katika mitandao mbalimbali ya kimataifa kote duniani.



 

Kwa kifupi:-

Kompyuta ni mashine au chombo cha kielektroniki chenye uwezo wakupokea taarifa, kufanya mahesabu, kushughulikia/kufanyia kazi na kutoa matokeo ya kazi hiyo na namna ilivyondeshwa, nakutoa matokeo ya kitu kilichofanyika/kinachoonekana.

Pia huhifadhi taarifa na kuwasiliana na watu na kompyuta nyingine. "Taarifa" inawezakuwa katika michoro, alama, nembo, tarakimu, sauti au lugha ya maandishi.

Kompyuta imegawanyika katika sehemu kuu mbili:
a.   Sehemu zisizoshikika (Software)
b.  Sehemu zinazoshikika (Hard ware)
Mtumiaji (User):

Kimsingi mtumiaji ni mtu yeyote anayetumia kompyuta, lakini kiutaalamu inaleta maana kama mtumiaji angalao awe mwenye ufahamu wa msingi juu ya matumizi ya kompyuta.

Pia mtumiaji huwasilianana Programu (software) zilizomo ndani yake na zile programu huwasiliana na sehemu zinazoshikika (hardware) na hapo mfumo mzima wa kimatumizi hukamilika.
Sehemu zisizoshikika
(software)
:
Ni muundo wenye mfumo wa maelekezo ambao hupewa kompyuta ilikufanya kazi maalumu.

Mfumo huu unaweza kugawanyika katika sehemu kuu mbili kama ifuatavyo:
1.  Mfumo wa kimatumizi (application sotfware:)

Katika matumizi (applications) tunapata microsoft word, kwa ajili ya kuandikia barua na nyaraka mbalimbali, Excel na Access kwa ajili ya kupangilia/kuandalia data na kufanyia mahesabu.

Hii inajumuisha Matumizi maalumu ya kiofisi (microsoft office), Mfumo wa ulipaji mishahara (payroll) na mfumo wa kihasibu (accounting system) na kadhalika.
2.    Ya pili ni muundo wa undeshaji (system software:)

Hii inajumuisha mfumo mzima wa undeshaji katika kompyuta.
Mfano wa mifumo (system) ni kama windows,Mac Operating
System, dos.