Sunday, April 17, 2016

COMPUTER GUIDE "JIFUNZE MWENYEWE" SEHEMU YA 2

Sehemu zinazoshikika
(Hardware)
:
Sehemu zinazoshikika (
Hardware:)

Ni aina zote za vifaa vya kielektroniki katika kompyuta.

Kuna aina tano za vifaa vinavyoshikika:

a.   Vifaa vya kuingiza nguvu ndani ya kompyuta au kifaa chochote kitumiacho umeme (input devices) kama kibodi (keyboard), mausi (mouse) na Kipaza sauti/microphone
b.   Vifaa vya uendeshaji, kama sakiti (circuits).

Hivi vipo ndani ya chombo kiitwacho Central Processing Unit (C.P.U.) ambacho ndicho kinachounganishwa na skrini na kuwa skrini hupata maelekezo yote kutoka kwenye C.P.U.
C.P.U. ni sehemu kuu ya nguvu za kompyuta, au kitovu cha kompyuta.
c.   Vifaa vya Kuhifadhia/kuhifadhi ni kama hadi diski/hard disk (ndani ya CPU), flopi diskifloppy diski draivu/disk drive na CD diski draivu/CD disk drive.
Hizi zina ni sehemu zinayotunza kumbukumbu (Memory).
d.  Vifaa vya kutoa, kama Skrini/kioo cha kompyuta (screen/monitor) na Kichapishio/printer.
e.   Vifaa vya kuwasiliana kama modemu/modem na kebozi/cables.



Utajifunza zaidi kwenye sehemu ya Vifaa.
Kwa mifano na maelezo zaidi bonyeza hapa.