Huu ni mfululizo wa mambo chungu nzima
ambayo utakutana nayo unapotaka kununua kompyuta mpya.
Kununua kompyuta si jambo rahisi. Kuna
aina nyingi mno za kompyuta. Unapaswa kwa kweli kununua kompyuta ambayo ni
sahihi kwako ili usije kujuta baadaye.
Kwamba baada ya mwaka mmoja tu
unajikuta haitoshelezi tena mahitaji yako.
Si kila kompyuta
inatengenezwa sawa
Kompyuta hazitengenezwi kwa usawa. Na
pia mahitaji ya mtu hayawezi kufanana na ya mwingine. Kwa hivyo manunuzi ya PC
mpya yanategemeana na mahitaji yako.
Kama unataka kompyuta yenye uwezo
mkubwa, itakubidi kulipa fedha nyingi zaidi. Katika muongozo huu, nitakuonesha
ni kwa jinsi gani viungo vilivyo ndani ya kompyuta vina maana gani kwako.
Hii itakusaidia kuamua unahitaji nini
na ni mambo yapi uyazingati zaidi.
Ni kwa jinsi hii ndiyo utaweza kuwa
katika nafasi nzuri ya kununua kompyuta inayokufaa na inayoendana na mahitaji
yako. Utakuwa katika nafasi ya kuepuka kutumia fedha nyingi pasipo sababu.
Unataka Kompyuta
Mpakato (Laptop) au ya Mezani (Desktop)?
Pengine huu ni uamuzi rahisi kwako.
Lakini pia ni uamuzi ambao utapelekea
kuamua ni kiasi gani utatumia kununua kompyuta yako. Kwa sababu kama Laptop na
Desktop zina uwezo unaolingana, laptop itakuwa aghali zaidi ya desktop.
Kwa nini?
Kwa sababu laptop ina sifa za ziada
ambazo desktop haina. Laptop inaweza kubebwa mahali popote kwa sababu ina umbo
dogo kuliko desktop. Laptop ni nyepesi zaidi ya desktop. Laptop ina betri
ambayo inaiwezesha kutumika hata mahali pasipo na umeme.
Desktop
Laptop
Kwa hivyo kama unataka kompyuta ambayo
itatumika zaidi mahali pamoja bila haja ya kubebeka, nunua desktop.
Desktop pia ina faida ya kwamba una uwezo wa kuitunza kwa uda mrefu zaidi ya
laptop. kwa sababu ina nafas kubwa ya kupoza joto na hivyo kuwa na maisha
marefu.
Pia ni rahisi kubadili au kuongeza
vifaa katika desktop kuliko katika laptop. hii inakupa mwanya wa kuboresha
kompyuta yako kutokana na mahitaji ya wakati husika hata kama umepita muda
mrefu.
Kwa hivyo kama unahitaji kusafiri mara
kwa mara, chagua laptop. Kumbuka pia kwamba kama mahitaji yako ni mambo madogo
madogo kama vile kutuma na kupokea email au kutafuta taarifa mtandaoni, unaweza
kununua kifaa cha mkononi (tablet) au hata laptop ndogo zaidi.
Lengo lako ni kusave fedha ambazo
zitatumika katika shughuli nyingine.
Hasa katika kipindi hiki cha utumbuaji
majipu.
Fahamu ubongo wa
kompyuta unayotaka kununua
Ubongo?
Yeah.
Ubongo wa Kompyuta –
CPU
Kompyuta ina ubongo ambao huendesha
kila kitu, kama vile ubongo wako unavyokusimamia wewe. Ubongo wa kompyuta
unaitwa processor, au central processing unit – CPU.
Kama unataka kompyuta yenye kasi,
inayowashwa na kuwa tayari kwa haraka, na inayokamilisha kile unachoiambia kwa
haraka, bila kuchelewa, basi nunua ile yenye CPU bora zaidi.
Utajuaje?
CPU hupimwa kwa kiwango cha Gigahertz –
GHz. Kompyuta nyingi za siku hizi huwa zimebandikwa nembo inayoonesha uwezo wa
CPU. Kadiri uwezo wa CPU unavyokuwa mkubwa ndiyo kiwango cha kuchakata taarifa
kwa haraka kinavyoongezeka.
Picha hii utaiona ikiwa imebandikwa
pembeni au ubavuni mwa kompyuta. Kompyuta nyingi siku hizi utaona zimebandikwa
nembo zinazosema core i3, core i5, au core i7.
Core i7 maana yake CPU ina uwezo mkubwa
zaidi kuliko core i5 na core i3. Hata hivyo kitaalam, kompyuta zenye core i3
zinatoa kelele hafifu kuliko zile zenye core i5 na core i7.
Uwezo wa nafasi ya
kufanyia kazi (RAM)
Kiwango cha uwezo wa kuhifadhi taarifa
na data wakati kompyuta ikifanya kazi kinaitwa RAM – Random access memory.
Ni kama vile tulinganishe chumba kidogo
ambacho wanaishi watu 10 na uwanja wa mpira ambako watu 60,000 wanaweza kuenea
kwa wakati mmoja.
Kadiri kompyuta inavyokuwa na RAM kubwa
ndivyo inavyoongezeka uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Watu kumi
watakaa kwa kujibana chumbani lakini ukiwachukua na kuwaweka katika uwanja,
watajitanua watakavyo.
RAM ya Kompyuta
Nunua kompyuta yenye RAM kubwa zaidi.
Kompyuta nyingi za kisasa zina RAM yenye Gigabyte 4 (4 GB) na kuendelea.
Unapokuwa na kompyuta yenye RAM kubwa, unakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa
haraka zaidi.
Kwa sababu kompyuta ina uwezo wa
kushughulikia kazi nyingi kwa wakati mmoja.
Pia RAM zinatofautina, hata kama zote
zina kiwango cha 4GB, kwa mfano. RAM yenye nembo DDR2-800 ina ufanisi mkubwa
zaidi ya RAM yenye nembo ya DDR2-400.
Kadiri ukubwa wa RAM unavyoongezeka,
ndivyo bei hupanda.
Uliza dukani kabla hujanunua.
Uwezo wa kutunza
kumbukumbu (Hard Drive au Hard Disk)
Kila kompyuta inahitaji sehemu ya
kutunza kumbukumbu – data storage. Sehemu hii ya kutunza kumbukumbu inaitwa hard
disk au hard drive – kwa kifupi HDD.
Kompyuta nyingi siku hizi zinaanzia na
HDD zenye ukubwa wa Gigabyte 500.
Unapochagua kompyuta, angalia mahitaji
yako. Una mpango wa kuhifadhi data nyingi au kompyuta yako ni kwa ajili ya
matumizi ya kawaida tu? Hii itakusaidia kupunguza bei ya kompyuta kwani kwadri
inavyokuwa na HDD kubwa ndivyo bei inavyoongezeka.
HARD DISK |
EXTERNAL HDD |
FLASH DISK |
Kumbuka pia kuwa teknolojia imeendelea
sana siku hizi. Kama huna fedha za kutosha lakini ungependea kuwa na sehemu
kubwa zaidi ya kuhifadhi data, kuna vifaa vya ziada – peripheral devices.
Flash disks
na External Hard Disk ni vifaa amnavyo unaweza kununua baadaye endpao
mahitaji yako yataongezeka.
Angalia mahitaji au
vifaa vya ziada – peripherals
Kuna vifaa gani vya ziada utavihitaji
katika kompyuta yako? Unataka kompyuta yako uweze kufanya nini?
Hapa utatambua unahitaji vifaa vya
ziada katika kompyuta yako kwa kutegemea utakavyoitumia kompyuta yako. Hebu
tutazame baadhi ya mambo ya ziada:
Matundu ya USB – Universal Serial Bus
(USB) slots.
Haya ni matundu kwa ajili ya kupachika
vifaa muhimu katika kompyuta kama vile kipanya (mouse), keyboard, kipaza sauti,
radio, na monitor. Matundu haya kwa hakika yanaweza kuunganisha kitu chochote
cha kielektroniki.
USB Ports |
Matundu ya USB